Donald Trump amechapisha tena picha ya wanawake wanane wa Iran wanaodaiwa kuwa katika hatari ya kunyongwa na kuwataka waachiliwe huru.
Kupitia mtandao wake wa Truth Social, aliandika: “Kwa viongozi wa Iran ambao hivi karibuni wataanza mazungumzo na wawakilishi wangu, nitashukuru sana kwa kuachiliwa huru wanawake hawa.”
Aliongeza: “Tafadhali msiwadhuru, na hili litakuwa mwanzo mzuri wa mazungumzo yetu.”
Mwishoni mwa Januari, kabla ya vita kuanza, rais huyo wa Marekani aliwashukuru viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kile alichokiita “kufutwa kwa hukumu za kunyongwa kwa zaidi ya watu 800.”
Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Iran amezitaja kauli hizo kuwa hazina msingi wowote.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!